Wednesday, October 30, 2024
Tuesday, October 8, 2024
MWAKA WA 587 K.K.

Shalom wapendwa watu wa Mungu ni mimi pastor victory karibu tujifunze pamoja Neno la Mungu Amen! Mwaka 587 k.k Babeli walibomoa mji wa Jerusalem,wakauharibu ufalme wa Yuda wakateka nyara mali yote na kuwapeleka watu waliofaa kifungoni huko Babeli, 2fal 25:1-21. Baada ya ufalme wa Yuda kuharibiwa wakamweka Gedalia,mwana wa afisa mmoja huko Yerusalemu awe mtawala wa wenyeji wa Yuda waliobaki nchini 2fal 25:22 taz.Yer 26:24. Ufalme mpya uliweka makao yake makuu mispa kaskazini mwa Yerusalemu.na kwa msaada wa nabii Yeremia,alifuata siasa ya kujikabidhi na kutii amri ya watu wa Babeli.hivyo hakuchukua hatua dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Yuda waliotoroka kifungoni na waliowapinga wa Babeli,bali aliwatia moyo pamoja na watu wengine wa Yuda waliotoroka kutoka kifungoni ili wahamie karibu na mispa 2fal 25:23-24 tz.Yer 40:5-12. Jemedari mmoja wa jeshi la zamani la Yuda,jina lake Ishmaeli,huyu alipinga siasa ya kuwatii babeli akafanya njama ya kumpindua Gedalia. Gedalia alipoambiwa habari zile hakuamini. Ishmael akamwinukia Gedalia pamoja maafisa wengine wa kiyahudi na wababeli waliokuwa makao makuu ya inchi.tz 2fal 25:25;Yer 40:13-41:3 huo ukawa mawazo wa mfululizo wa matukio yaliyoleta hofu kwa wayahudi wakaogopa sana kisasi cha wababeli ndipo wayahudi waliobaki wakakimbilia Misri tz 2fal 25:26;Yer 41;4-43:13. Katika biblia tunaona watu wengine wanne walioitwa Gedalia. Mfano; wa kwanza alikuwa mtaalamu wa muziki wakati wa Daudi tz 1nyak 25:3,9. Wa pili alikuwa babu wa nabii Sefania tz Sef 1:1,wa tatu alikuwa afisa wa Yerusalemu aliyempinga Yeremia,tz Yer 38:1-6 na wa nne alikuwa Kuhani wakati wa Ezra tz Ezra 10:18. Bwana akubariki kwa kufuatana nami katika somo hili Bwana awabariki sana. Ungependa kuwasiliana nami kwa ushauri maombi na maombezi karibu tuwasiliane kwa: pastorvictorykilugumablogspot.com au 0612083598.pia napenda kuwakaribisha kwa ujenzi wa kanisa hapa lringa Agape pentecoste church unaoendelea kwa bishop victory kiluguma tunapokea sadaka ya mchango wako kwa akaunt namba NMB BANK 60510090270 au Halopesa 0612083598 victory kiluguma. Nyote mnakaribishwa.
Friday, September 13, 2024
MAFUNZO YA UONGOZI NI MSINGI MKUBWA KATIKA KUJENGA MAISHA BORA YA KIKRISTO
Shalom wa pendwa katika Yesu kristo mwokozi wetu. Kitabu cha kwanza na cha pili cha Timotheo ni vitabu vinavyo funua ukweli kuhusu uongozi wa kichungaji. Nyaraka hizi mbili zinatuonesha wachungaji watumishi wa Yesu kristo ambao wamefundishwa na Mungu kukaa katika kweli ya Neno la Mungu. 1tim 3:15 mtume Paulo anamwambia Timotheo nakuandikia upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Mtume Paulo anasema na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha wengine " 2tim 2:2. Katika safari ya kwanza ya umisheni,Paulo alienda katika mji uitwao listra. Huko alikuwako kijana aliyekuwa akiishi huko aliitwa Timotheo. Paulo mtume akakutana naye kijana Timotheo pamoja na familia yake. Bibi na mama yake Timotheo familia hii walimpokea kristo kuwa mwokozi wao.baadae tena katika safari ya tatu huko listra mtume aliitembelea familia ya Timotheo na kumwalika Timotheo kuungana naye katika safari zake za umisheni. Timotheo akiwa kijana mkubwa alikubali kuwa mmishenari pamoja na Paulo mtume, Paulo akamwita Timotheo nakuwa kijana wake Paulo katika imani maana, alimwongoza kumfahamu Bwana. Paulo mtume alimpenda kijana Timotheo alikuwa kijana aliye mwamini Mungu imani iliyotokana na bibi yake na mama yake 2tim 1:5- baadae anajifunza kumtumikia Bwana kutoka kwa Baba wa kiroho mtume Paulo. Timotheo alikuwa na mwonekano mzuri kwa watu waliomwani Mungu katika mji wa listra na watu walimshuhudia mema. Mate 16:2 baadae sana mtume paulo akiwa gerezani anamwandikia waraka akikumbuka huruma na upendo wa kweli aliokuwa nao kijana Timotheo. mtume Paulo alifurahi mno alipomkumbuka Timotheo. 2tim 1:4. Baadae Paulo anatoka gerezani anamchukua Timotheo anamfundisha kumtumikia Bwana anasafiri naye katika huduma. Timotheo anamwona mtume Paulo akihubiri injili na kufundisha wakristo wapya. na kuwaongoza katika kweli yote ya Mungu. Timotheo anamwona mtume Paulo ni baba wa kiroho na Mwalimu wake wa imani. Mtume Paulo alifungua makanisa mapya, akiwafundisha wakristo wachanga kiroho akiwaimarisha katika imani na kuwaongoza. Mtume Paulo anamwona Timotheo ni kijana anaye penda kujifunza,anafuata kanuni ya imani, ni mwaminifu,katika mafundisho, mtume Paulo anamweka Timotheo kuwa mchungaji wa kanisa la efeso. Kazi ya Bwana aliyo kabidhiwa Timotheo ilikuwa ikiendelea kukua, Paulo na Timotheo wakaendelea kumtumikia Mungu pamoja kwa upendo kama baba na mwanae. Katika imani ya kristo. Timotheo alibaki katika mji wa efeso akifundisha na kuchunga kundi la Mungu. katika siku zile kulikuwa na hatari maana walitokea watu waliojifanya waalimu wa uongo 1tim 1:6-7 waliamu hawa walifundisha uongo. Kwa sababu hii alihitajika mtu ambaye angeweza kuwazuia, na kufichua hila yao, kwa kuwafundisha watu wa Mungu Neno la Mungu kwa usahihi kabisa.ili watu wote waijue kweli yote ya Mungu. Paulo anamwona mchungaji Timotheo angeweza kufanya hivyo. 1 tim 1:3-4. Mtume Paulo anasisitiza wetu waishike ile imani ya kweli. Ni jukumu la kila mchungaji kuliongoza kanisa, katika kweli, ya yote ya Mungu. Ni lazima mchungaji aihubiri injili ya kweli kwa uaminifu, na zaidi sana lazima mchungaji aiishi hiyo kweli mbele za Mungu na watu anaowaongoza. Haleluya! watu wa Mungu! Naami ujumbe huu utafanyika baraka kwako! Bwana awabariki nyote. Mtayarishaji ni mimi mtumishi wa Mungu Victory chalres kiluguma kutoka Agape sanctuary christian pentecoste Jerusalem lringa. Ungependa kuwasiliana nami niandikie; pastorvictorykiluguma@blogspot.com au victorykiluguma80@gmail.com au nipigie simu 0612083598. Amen!Sunday, September 1, 2024
Wednesday, August 28, 2024
MIKUTANO YA INJILI MWEZI WA 8
Shalom watu wa Mungu Mungu ni mwema namtukuza Bwana mno ametusaidia kuwa na mfululizo wa mikutano ya injili, Agost, lringa kitayawa mikutano miwili, lringa Kilolo mkutano mmoja, mkoa wa Kilimanjaro tumekuwa na mkutano mkubwa wa injili, wa siku 5 njia panda ya himo stand, na sanya juu nasai mkutano wa kufungua tawi la New life Himo kwa siku 3 na ufunguzi wa Kituo kikuu cha New life Tanzania prayer centre Himo kwa mchungaji Rafael. Amen Bwana awabariki nyote! Ni mimi victory kiluguma askofu wa Agape sanctuary Pentecostel lringa Centre Kitayawa. Kwa mawasiliano: pastorvictorykiluguma@blogspot.com. au nipigie 0612083598 au niandikie victorykiluguma@gmail.com.
Sunday, August 18, 2024
GOD BLESS YOU ALL
Thursday, August 15, 2024
AGAPE SANCTUARY CHURCH'S INTENATIONAL PENTECOSTEL JERUSALEMU CHRISTIAN CENTER IRINGA
Wednesday, August 7, 2024
MKUTANO WA INJILI UNAENDELEA

Tunamshukuru Mungu leo jumatano ni siku ya 3 tangu mkutano uanze hapa lringa kitayawa katika viwanja vya Kanisa la Agape sanctuary Pentecostel kwa askofu victory kiluguma.wachungaji wa makanisa ya kipentekoste wanashiriki mkutano huu wa Baraka tunamwona Mungu watu wanaokolewa wanafunguliwa na kuponywa na Bwana Yesu. Utukufu kwa Mungu wetu. Nyote mnakaribishwa shalom.ni mimi mtumishi victory kiluguma askofu. Karibuni sana!
Thursday, August 1, 2024
Tuesday, July 30, 2024
TUOMBEE TAIFA LETU TANZANIA
![]() |
Tuwaombee Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya wote viongozi wote waserikali inchini.tuwaombee watanzania wote, Tuwaombee maaskofu Wakuu,maaskofu wa majimbo,au mikoa maaskofu,wa wilaya na Wachungaji wote.Tuliombee kanisa la Mungu Tanzania.MITHALI 12:10-11, WENYE HAKI WASTAWIPO,MJI HUFURAHI;WAOVU WAANGAMIAPO,WATU HUPIGA KELELE.11 MJI HUTUKUZWA KWA MBARAKA WA MWENYE HAKI.YOHELI 2:17 HAO MAKUHANI,WAHUDUMU WA BWANA,NA WLIE KATI YA PATAKATIFU NA MADHABAHU,NAACH,WASEME,WASEME, WALA USIUTOE URITHI WAKO UPATE AIBU,HATA MATAIFA WAWATAWALE JUU YAO;KWANI WASEME,KATI YA WATU,YUKO WAPI MUNGU WAO? 18 HAPO NDIPO BWANA ALIPOONA WIVU KWAAJILI YA INCHI YAKE AKAWAHURUMIA WATU WAKE.19 BWANA AKAJIBU,AKAWAMBIA WATU WAKE;TAZAMENI,NITAWALETEA NAFAKA,NA DIVAI,NA MAFUTA,NANYI MTASHIBA KWA VITU HIVYO;WALA SITAWAFANYA WAKE; LA KASKAZINI NITALIONDOLEA MBALI NANYI,NAMI NITALIFUKUZA MPAKA INCHI YA UKAME NA UKIWA;SEHEMU YAKE YA MBELE ITAINGIA KATIKA BAALI YA MAGHARIBI;NA UVUNDO WAKE UTAPANDA JUU,NA HARUFU YAKE MBAYA ITAPANDA JUU,KWA SABABU AMETENDA MAMBO. 21 Ee INCHI USIOGOPE; FURAHI NA KUSHANGILIA, KWA KUWA BWANA AMETENDA MAMBO MAKUBWA.AMEN! ungependa kuwasiliana nami kwa ushauri na maombi karibu Nipigie kwa 0612083598 au niandikie pastorvictorykiluguma@blogspot.com Amen Bwana awabariki sana
Monday, July 22, 2024
MKUTANO WA INJILI IRINGA
AGAPE PENTECOSTE JERUSALEMU CHRISTIAN CENTRE KITAYAWA IRINGA.KWA ASKOFU VICTORY KILUGUMA. TUNAYOFURAHA KUWAKALIBISHA NYOTE KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UTAKAOFANYIKA TAR 8/8/2023/HADI TAR 11/8/2023 BWANA AWABARIKI SANA
Thursday, July 18, 2024
Wednesday, July 17, 2024
Tuesday, July 16, 2024
WOKOVU SEHEMU YA PILI
Bwana Yesu akubariki ni mimi mtumishi wa Mungu victor kiluguma karibu tuendelee na sehemu ya pili ya somo letu ujue wokovu; Wokuvu tunaupata kwa Neema ya Mungu.wokovu hatupati kwa kujitahidi kwetu kufanya matendo mema,mbele za Mungu na wanadamu, Tito 3:4-7 Mungu anatuona sisi kuwa sisi tu Roho moja na Bwana Yesu 1kor 6:17 lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni Roho. . moja naye. sababu hii sisi tu watoto wake tumepatikana kwa kifo cha Yesu msalabani. ile damu ya thamani ya mwana wa Mungu Yesu imetutakasa na kutufanya wa thamani mbele za Mungu 1pet 1:18-19. Zaburi 2:8. Tulipo okoka tumepewa mamlaka ya kutumia jina la Yesu. Wafilipi 2:9-11. sisi tu mali ya Mungu na vyote tulivyo navyo. 1kor 6:19-20,1kor 4:1-2 baada ya kuokoka tu mawakili wa siri za Mungu. Maombi: kwa nini tuombe? Mungu anatupenda hata akatuokoa kwa neema yake kuu hawezi kutupa mahitaji yetu sisi kuomba? Mungu anajua mahitaji yetu yote hata hatujanwsmbia Mungu anatupenda sana. Kwa nini basi asitupe tu mahitaji yetu? Mbona anataka sisi tumwombe? Yafuatayo ni majibu ya maswali haya ambayo naamini wengi wanajiuliza. Bwana YESU ametufundisha tuombe Bwana atafanya Luk 11:9-10 Bwana Yesu mwenyewe alimwomba Mungu sana apewe nguvu na Mungu baba ili akamilishe huduma ya ukombozi wa mwanadamu hapa duniani. Waebr 5:7-10 tunasoma Yeye siku hizo za mwili wake alimtolea yule, aweza kumwokoa na kumtoa katika mauti,maombi na dua pamoja na kulia sana kwa machozi,akisikilizwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;na ingawa ni mwana,alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa,akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;kisha ametajwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa melkizedeki. Matendo 6:4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile neno. Tudumu katika kuomba kama Bwana YESU na mitume walivyo omba. Yakobo 5:16 kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana,akiomba kwa bidii. Jinsi ya kuomba: tunaombaje? tunaomba kwa imani kutoka ndani ya Roho, si kwa maneno ya mdomoni yaliyopangwa vizuri kiakili tu, mat 6:6 maneno yanayotoka mdomoni yanatuunganisha na Mungu anayeyasikiya pia tunaweza kuomba kwa sauti kubwa ya kusikika tukiwa pekee yetu, au tukiwa wengine kama kanisani tukiomba pamoja. , Matendo 4:24 . Mungu si mwanadamu hata akachanganyikiwa kwa maombi ya watu wengi pamoja wakati mwingine wakimwomba Mungu kila jambo tofauti alivyo wa ajabu kila mmoja humsikia ombi lake na kumjibu kwa majira yake, hata kama wengine wanaomba huko ulsys,Asia,America na Africa. mbalimbali kwa wakati mmoja Mungu huwasikia wote kwa wakati mmoja. Je naweza kuomba kwa sauti ndogo sana ambayo wengine hawasikii isipokuwa mimi tu,na Mungu akanisikia? Jibu ni ndiyo. 1Samwer 1:10-17 yapo mazingira yanayotulazimu tuombe kwa sauti ndogo.Mungu hatusikii kwa kuwa tumeomba kwa sauti ndogo au kubwa. Mungu anatusikis kwa sababu tumeomba kwa imani. Je nasikia kuomba kwa kulia machozi hivi ni sawa jibu ni sawa kabisa. Bwana wetu Yesu aliomba kwa machozi kwa kulia sana. Ebra 5:7-9. Tusiogope kuwa wetu watasema nini tuombe tu kwa imani tufaham kuwa Mungu hutusikis na kutujibu. Shalom naamini somo hili limefanyika baraka kwako mtu wa Mungu naamini unachukua hutua kuwa mwombaji wa kiwango cha juu cha imani ndani ya Yesu kristo. nami nakuombea Bwana akusikie na kujibu maombi yako in Jesus name. ni mimi ushindi kiluguma bishop from lringa Tanzania karibu kwa somo lijalo na Mungu akubariki sana shalom kwa maombi na ushauri tuwasiliane kwa simu 0612083598 au pastorvictorykiluguma@blogspot.com
Monday, July 15, 2024
UJUE WOKOVU
UJUE WOKOVU: shalom ni mimi mchungaji victor ninayo furaha kubwa kukuletea ujumbe wa baraka yaani ujue wokovu. Tunapojifunza kukulia wokovu ni muhimu sana kuelewa maana ya wokovu wenyewe. Wokovu ni tendo la Mungu kwetu sisi wanadamu na sio sisi wanadamu kujiokoa wenyewe.mpendwa mtu wa Mungu WARUMI 10:9-10 imeandikwa kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako cha kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. . 10 kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe asipotuokoa sisi kwa Neema yake, kamwe hatuwezi kuokoka. HATUA YA KUAMINI NA KUKIRI ili uweze kukiri na kuamini na kukiri, imetupasa kusikia Neno la Mungu. Mpendwa mtu wa Mungu WARUMI 10:17, imeandikwa Basi imani chanzo chake ni kusikia: na kusikia huja kwa Neno la kristo. Tunaposikia Neno la kristo ndani yetu kunaumbika imani ya kristo. WARUMI 8:1,10:8-10, 2KOR 7:10. HATUA YA KUPOKEA MSAMAHA WA DHAMBI . Baada ya kutubu mbele za Mungu imetupasa kuamini kuwa Mungu ametusamehe dhambi zetu zote kabisa.Hakumbuki tena, nasisi tusiendelee kuzikumbuka EZEKIEL 18:21-22, imeandikwa, lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa, dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mmoja; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Haleluya! Bwana Yesu asifiwe. Tujue sasa kuwa hatuna hukumu kwa ajili ya dhambi tena 1YOH 1:9-10 tunapo jua tumemkosea Mungu kwa kufanya dhambi,hapo inakupasa kutubu kwa Mungu upesi,na Mungu mwenye Rehema atakusamehe 1YOH 1:9. TAHADHARI: WAEBRANIA 6:4-6. Imeandikwa kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru,na kuonja kipawa cha mbinguni, na ushirika wa Roho matakatifu,na kulionja Neno zuri la Mungu,na nguvu za zamani za baadaye,wakaanguka baada ya hayo,haiwezekani kufanya upya tena hata watubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao,na kumfedhehi kwa dhairi. KUFANYIKA KUWA MTOTO WA MUNGU. Tufahamu kuwa tunafanyika watoto wa Mungu kwa nguvu za Mungu mwenyewe, yaani Mungu mwenyewe anatufanya watoto wake. Hatuwezi kujifanya watoto wa Mungu. Mpendwa mtu wa Mungu YOHANA 1:12 imeandikwa Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Mpendwa mtu wa Mungu naamini somo hili limefanyika baraka kwako. Basi tukatane wakati mwingine nitakapo letea sehemu ya pili ya somo hili Bwana akubariki sana! Ni mimi victor kiluguma askofu kutoka agape pentecoste lringa Tanzania. Kwa maombi na ushauri tuwasiliane kwa blog hii pastorvictorykiluguma@blogspot.com au kwa gmail:victorykiluguma80@gmail.com au kwa simu 0612083598.
Monday, July 8, 2024
MPANGO WA MUNGU KUKUFANIKISHA NA KUKUSTAWISHA. ZEKARIA 1:17. piga kelele tena na kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, kwa kufanikiwa itaeneza huko na huko tena; Naye Bwana ataufajili sayuni tena,atauchagua yerusalemu tena. ZABURI 122:6-9 utakieni yerusalemu amani na wafanikiwe wakupendao amani na ikae ndani ya kuta zako na kufanikiwa ndani ya majumba yako. Kwa ajili ya ndugu zangu na Rafiki zangu. Niseme sasa amani ikae nawe kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu. ZABURI 35:27 washangilie na kufurahi, wapendezwao na haki yangu. Naam waseme daima atukuzwe Bwana, apendezwae na amani ya Mtumishi wake. AYUBU 36:11. Kama wakisikia na Kumtumikia watapisha siku zao katika kufanikiwa, na miaka yao katika furaha. YOSHUA 1:8 kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako,bali tafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako,kisha ndipo utakapo sitawi sana. HALELUYA NAAMINI UJUMBE HUU UMEFANYIKA BARAKA KWAKO MSOMAJI MTU WA MUNGU BWANA AKUBARIKI NAMI NAKUOMBEA UFANIKIWE NA KUSITAWI KWA JINA LA YESU KRISTO. MUNGU ALIE HAI MUUMBA NA MWOKOZI AKATHIBITISHE NENO LAKE KATIKA MAISHA YAKO. BWANA AKUBARIKI SANA IWAPO UNEPENDA USHAURI AU MAOMBI TAFADHALI NIANDIKIE KWA GMAIL: winningkiluguma80@gmail.com au nipigie kwa 0612083598 au kwa blog hii pastorvictorykilugumablogspot
Saturday, June 22, 2024
Hello welcome l am pastor Victory Kiluguma nawapenda nyote
Haleluya Bwana Yesu asifiwe karibu katika blog hii upate Barikiwa kwa mafundisho ya neno la Mungu na maombi na maombezi ni mimi mchungaji ushindi katika kanisa la agape pentecoste lringa Tanzania. Karibuni wote Bwana Awabariki sana
























