WOKOVU SEHEMU YA PILI
Bwana Yesu akubariki ni mimi mtumishi wa Mungu victor kiluguma karibu tuendelee na sehemu ya pili ya somo letu ujue wokovu; Wokuvu tunaupata kwa Neema ya Mungu.wokovu hatupati kwa kujitahidi kwetu kufanya matendo mema,mbele za Mungu na wanadamu, Tito 3:4-7 Mungu anatuona sisi kuwa sisi tu Roho moja na Bwana Yesu 1kor 6:17 lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni Roho. . moja naye. sababu hii sisi tu watoto wake tumepatikana kwa kifo cha Yesu msalabani. ile damu ya thamani ya mwana wa Mungu Yesu imetutakasa na kutufanya wa thamani mbele za Mungu 1pet 1:18-19. Zaburi 2:8. Tulipo okoka tumepewa mamlaka ya kutumia jina la Yesu. Wafilipi 2:9-11. sisi tu mali ya Mungu na vyote tulivyo navyo. 1kor 6:19-20,1kor 4:1-2 baada ya kuokoka tu mawakili wa siri za Mungu. Maombi: kwa nini tuombe? Mungu anatupenda hata akatuokoa kwa neema yake kuu hawezi kutupa mahitaji yetu sisi kuomba? Mungu anajua mahitaji yetu yote hata hatujanwsmbia Mungu anatupenda sana. Kwa nini basi asitupe tu mahitaji yetu? Mbona anataka sisi tumwombe? Yafuatayo ni majibu ya maswali haya ambayo naamini wengi wanajiuliza. Bwana YESU ametufundisha tuombe Bwana atafanya Luk 11:9-10 Bwana Yesu mwenyewe alimwomba Mungu sana apewe nguvu na Mungu baba ili akamilishe huduma ya ukombozi wa mwanadamu hapa duniani. Waebr 5:7-10 tunasoma Yeye siku hizo za mwili wake alimtolea yule, aweza kumwokoa na kumtoa katika mauti,maombi na dua pamoja na kulia sana kwa machozi,akisikilizwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;na ingawa ni mwana,alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa,akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;kisha ametajwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa melkizedeki. Matendo 6:4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile neno. Tudumu katika kuomba kama Bwana YESU na mitume walivyo omba. Yakobo 5:16 kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana,akiomba kwa bidii. Jinsi ya kuomba: tunaombaje? tunaomba kwa imani kutoka ndani ya Roho, si kwa maneno ya mdomoni yaliyopangwa vizuri kiakili tu, mat 6:6 maneno yanayotoka mdomoni yanatuunganisha na Mungu anayeyasikiya pia tunaweza kuomba kwa sauti kubwa ya kusikika tukiwa pekee yetu, au tukiwa wengine kama kanisani tukiomba pamoja. , Matendo 4:24 . Mungu si mwanadamu hata akachanganyikiwa kwa maombi ya watu wengi pamoja wakati mwingine wakimwomba Mungu kila jambo tofauti alivyo wa ajabu kila mmoja humsikia ombi lake na kumjibu kwa majira yake, hata kama wengine wanaomba huko ulsys,Asia,America na Africa. mbalimbali kwa wakati mmoja Mungu huwasikia wote kwa wakati mmoja. Je naweza kuomba kwa sauti ndogo sana ambayo wengine hawasikii isipokuwa mimi tu,na Mungu akanisikia? Jibu ni ndiyo. 1Samwer 1:10-17 yapo mazingira yanayotulazimu tuombe kwa sauti ndogo.Mungu hatusikii kwa kuwa tumeomba kwa sauti ndogo au kubwa. Mungu anatusikis kwa sababu tumeomba kwa imani. Je nasikia kuomba kwa kulia machozi hivi ni sawa jibu ni sawa kabisa. Bwana wetu Yesu aliomba kwa machozi kwa kulia sana. Ebra 5:7-9. Tusiogope kuwa wetu watasema nini tuombe tu kwa imani tufaham kuwa Mungu hutusikis na kutujibu. Shalom naamini somo hili limefanyika baraka kwako mtu wa Mungu naamini unachukua hutua kuwa mwombaji wa kiwango cha juu cha imani ndani ya Yesu kristo. nami nakuombea Bwana akusikie na kujibu maombi yako in Jesus name. ni mimi ushindi kiluguma bishop from lringa Tanzania karibu kwa somo lijalo na Mungu akubariki sana shalom kwa maombi na ushauri tuwasiliane kwa simu 0612083598 au pastorvictorykiluguma@blogspot.com
No comments:
Post a Comment