UJUE WOKOVU: shalom ni mimi mchungaji victor ninayo furaha kubwa kukuletea ujumbe wa baraka yaani ujue wokovu. Tunapojifunza kukulia wokovu ni muhimu sana kuelewa maana ya wokovu wenyewe. Wokovu ni tendo la Mungu kwetu sisi wanadamu na sio sisi wanadamu kujiokoa wenyewe.mpendwa mtu wa Mungu WARUMI 10:9-10 imeandikwa kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako cha kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. . 10 kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe asipotuokoa sisi kwa Neema yake, kamwe hatuwezi kuokoka. HATUA YA KUAMINI NA KUKIRI ili uweze kukiri na kuamini na kukiri, imetupasa kusikia Neno la Mungu. Mpendwa mtu wa Mungu WARUMI 10:17, imeandikwa Basi imani chanzo chake ni kusikia: na kusikia huja kwa Neno la kristo. Tunaposikia Neno la kristo ndani yetu kunaumbika imani ya kristo. WARUMI 8:1,10:8-10, 2KOR 7:10. HATUA YA KUPOKEA MSAMAHA WA DHAMBI . Baada ya kutubu mbele za Mungu imetupasa kuamini kuwa Mungu ametusamehe dhambi zetu zote kabisa.Hakumbuki tena, nasisi tusiendelee kuzikumbuka EZEKIEL 18:21-22, imeandikwa, lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa, dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mmoja; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Haleluya! Bwana Yesu asifiwe. Tujue sasa kuwa hatuna hukumu kwa ajili ya dhambi tena 1YOH 1:9-10 tunapo jua tumemkosea Mungu kwa kufanya dhambi,hapo inakupasa kutubu kwa Mungu upesi,na Mungu mwenye Rehema atakusamehe 1YOH 1:9. TAHADHARI: WAEBRANIA 6:4-6. Imeandikwa kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru,na kuonja kipawa cha mbinguni, na ushirika wa Roho matakatifu,na kulionja Neno zuri la Mungu,na nguvu za zamani za baadaye,wakaanguka baada ya hayo,haiwezekani kufanya upya tena hata watubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao,na kumfedhehi kwa dhairi. KUFANYIKA KUWA MTOTO WA MUNGU. Tufahamu kuwa tunafanyika watoto wa Mungu kwa nguvu za Mungu mwenyewe, yaani Mungu mwenyewe anatufanya watoto wake. Hatuwezi kujifanya watoto wa Mungu. Mpendwa mtu wa Mungu YOHANA 1:12 imeandikwa Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Mpendwa mtu wa Mungu naamini somo hili limefanyika baraka kwako. Basi tukatane wakati mwingine nitakapo letea sehemu ya pili ya somo hili Bwana akubariki sana! Ni mimi victor kiluguma askofu kutoka agape pentecoste lringa Tanzania. Kwa maombi na ushauri tuwasiliane kwa blog hii pastorvictorykiluguma@blogspot.com au kwa gmail:victorykiluguma80@gmail.com au kwa simu 0612083598.
Monday, July 15, 2024
UJUE WOKOVU

No comments:
Post a Comment