Saturday, June 22, 2024

Hello welcome l am pastor Victory Kiluguma nawapenda nyote


Haleluya Bwana Yesu asifiwe karibu katika blog hii upate Barikiwa kwa mafundisho ya neno la Mungu na maombi na maombezi ni mimi mchungaji ushindi katika kanisa la agape pentecoste lringa Tanzania. Karibuni wote Bwana Awabariki sana

1 comment:

Pastorvictorykiluguma.blogspot.com said...

SHALOM KARIBU NI MIMI MCHUNGAJI VICTORY KILUGUMA NAMSHUKURU MUNGU KWA NAFASI HII NAOMBA TUBARIKIWE PAMOJA KWA NENO LA MUNGU . KARIBU SANA, NINA HABARI NJEMA NAYO NI HII MUNGU ANAKUPENDA. YOHANA 3:16 kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele. 17 maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili ahukumiwe ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.18 Amwaminie yeye haukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini Jina pekee la Mwana wa Mungu. WARUMI 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa kristo alikufa kwaajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi. BWANA YESU ASIFIWE!! TUONE SEHEMU YA PILI, DHAMBI HULETA MAUTI SOMA WARUMI 6:23 kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali Karama ya Mungu ni uzima wa milele katika kristo Yesu Bwana wetu. WARUMI 3:23 kwa sababu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; BWANA YESU ASIFIWE! UJUMBE SEHEMU YA TATU. JINSI YA KUTUBU DHAMBI. SOMA 1YOHANA 1:9 tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu,na kutusafisha na udhalimu wote. HALELUYA NAAMINI UMEBARIKI NA SOMO HILI NAKUSHAURI CHUKUA HATUA YA IMANI JE UNAPENDA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO? BASI SALI SALA HII NA YESU ATAKUJA NDANI YAKO AKUOKOE SASA HIVI SEMA. MUNGU BABA ASANTE KWA KUNIPENDA NAMPOKEA YESU SASA, BWANA YESU KARIBU NDANI YA MOYO WANGU UWE BWANA NA MWOKOZI WANGU NAKIRI KWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI NATUBU DHAMBI ZOTE NA KUZIACHA LEO YESU NISAIDIE NIOSHE KWA DAMU YAKO YA THAMANI BWANA YESU ASANTE KWA KUNISAMEHE NA KUNIOKOA AMEN! Haleluya hongera kwa Kuoka endelea kumpenda Mungu Naumtumikie (1)uende kanisani kila siku ya ibada ili umwabudu Mungu.(2)Soma Biblia Neno la Mungu kila siku na Umwombe Mungu ili ukue na kuimarika kiroho (3)ushirika, shirikiana na wakristo wenzako ili ujifunze namna ya kumwishia Mungu itakusaidia kukua na kuimarika zaidi katika imani (4)hubiri habari njema (lnjili) ya Yesu kristo kwa watu wote. Shalom Bwana akubariki sana! ni mimi mchungaji victory kiluguma

Post a Comment