Pastor victory kiluguma blog
Wednesday, October 30, 2024
Tuesday, October 8, 2024
MWAKA WA 587 K.K.
Shalom wapendwa watu wa Mungu ni mimi pastor victory karibu tujifunze pamoja Neno la Mungu Amen! Mwaka 587 k.k Babeli walibomoa mji wa Jerusalem,wakauharibu ufalme wa Yuda wakateka nyara mali yote na kuwapeleka watu waliofaa kifungoni huko Babeli, 2fal 25:1-21. Baada ya ufalme wa Yuda kuharibiwa wakamweka Gedalia,mwana wa afisa mmoja huko Yerusalemu awe mtawala wa wenyeji wa Yuda waliobaki nchini 2fal 25:22 taz.Yer 26:24. Ufalme mpya uliweka makao yake makuu mispa kaskazini mwa Yerusalemu.na kwa msaada wa nabii Yeremia,alifuata siasa ya kujikabidhi na kutii amri ya watu wa Babeli.hivyo hakuchukua hatua dhidi ya viongozi wa kijeshi wa Yuda waliotoroka kifungoni na waliowapinga wa Babeli,bali aliwatia moyo pamoja na watu wengine wa Yuda waliotoroka kutoka kifungoni ili wahamie karibu na mispa 2fal 25:23-24 tz.Yer 40:5-12. Jemedari mmoja wa jeshi la zamani la Yuda,jina lake Ishmaeli,huyu alipinga siasa ya kuwatii babeli akafanya njama ya kumpindua Gedalia. Gedalia alipoambiwa habari zile hakuamini. Ishmael akamwinukia Gedalia pamoja maafisa wengine wa kiyahudi na wababeli waliokuwa makao makuu ya inchi.tz 2fal 25:25;Yer 40:13-41:3 huo ukawa mawazo wa mfululizo wa matukio yaliyoleta hofu kwa wayahudi wakaogopa sana kisasi cha wababeli ndipo wayahudi waliobaki wakakimbilia Misri tz 2fal 25:26;Yer 41;4-43:13. Katika biblia tunaona watu wengine wanne walioitwa Gedalia. Mfano; wa kwanza alikuwa mtaalamu wa muziki wakati wa Daudi tz 1nyak 25:3,9. Wa pili alikuwa babu wa nabii Sefania tz Sef 1:1,wa tatu alikuwa afisa wa Yerusalemu aliyempinga Yeremia,tz Yer 38:1-6 na wa nne alikuwa Kuhani wakati wa Ezra tz Ezra 10:18. Bwana akubariki kwa kufuatana nami katika somo hili Bwana awabariki sana. Ungependa kuwasiliana nami kwa ushauri maombi na maombezi karibu tuwasiliane kwa: pastorvictorykilugumablogspot.com au 0612083598.pia napenda kuwakaribisha kwa ujenzi wa kanisa hapa lringa Agape pentecoste church unaoendelea kwa bishop victory kiluguma tunapokea sadaka ya mchango wako kwa akaunt namba NMB BANK 60510090270 au Halopesa 0612083598 victory kiluguma. Nyote mnakaribishwa.
Friday, September 13, 2024
MAFUNZO YA UONGOZI NI MSINGI MKUBWA KATIKA KUJENGA MAISHA BORA YA KIKRISTO

Sunday, September 1, 2024
Wednesday, August 28, 2024
MIKUTANO YA INJILI MWEZI WA 8
Shalom watu wa Mungu Mungu ni mwema namtukuza Bwana mno ametusaidia kuwa na mfululizo wa mikutano ya injili, Agost, lringa kitayawa mikutano miwili, lringa Kilolo mkutano mmoja, mkoa wa Kilimanjaro tumekuwa na mkutano mkubwa wa injili, wa siku 5 njia panda ya himo stand, na sanya juu nasai mkutano wa kufungua tawi la New life Himo kwa siku 3 na ufunguzi wa Kituo kikuu cha New life Tanzania prayer centre Himo kwa mchungaji Rafael. Amen Bwana awabariki nyote! Ni mimi victory kiluguma askofu wa Agape sanctuary Pentecostel lringa Centre Kitayawa. Kwa mawasiliano: pastorvictorykiluguma@blogspot.com. au nipigie 0612083598 au niandikie victorykiluguma@gmail.com.
Sunday, August 18, 2024
GOD BLESS YOU ALL
Thursday, August 15, 2024
AGAPE SANCTUARY CHURCH'S INTENATIONAL PENTECOSTEL JERUSALEMU CHRISTIAN CENTER IRINGA
Wednesday, August 7, 2024
MKUTANO WA INJILI UNAENDELEA

Tunamshukuru Mungu leo jumatano ni siku ya 3 tangu mkutano uanze hapa lringa kitayawa katika viwanja vya Kanisa la Agape sanctuary Pentecostel kwa askofu victory kiluguma.wachungaji wa makanisa ya kipentekoste wanashiriki mkutano huu wa Baraka tunamwona Mungu watu wanaokolewa wanafunguliwa na kuponywa na Bwana Yesu. Utukufu kwa Mungu wetu. Nyote mnakaribishwa shalom.ni mimi mtumishi victory kiluguma askofu. Karibuni sana!
Thursday, August 1, 2024
Tuesday, July 30, 2024
TUOMBEE TAIFA LETU TANZANIA
![]() |
Tuwaombee Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya wote viongozi wote waserikali inchini.tuwaombee watanzania wote, Tuwaombee maaskofu Wakuu,maaskofu wa majimbo,au mikoa maaskofu,wa wilaya na Wachungaji wote.Tuliombee kanisa la Mungu Tanzania.MITHALI 12:10-11, WENYE HAKI WASTAWIPO,MJI HUFURAHI;WAOVU WAANGAMIAPO,WATU HUPIGA KELELE.11 MJI HUTUKUZWA KWA MBARAKA WA MWENYE HAKI.YOHELI 2:17 HAO MAKUHANI,WAHUDUMU WA BWANA,NA WLIE KATI YA PATAKATIFU NA MADHABAHU,NAACH,WASEME,WASEME, WALA USIUTOE URITHI WAKO UPATE AIBU,HATA MATAIFA WAWATAWALE JUU YAO;KWANI WASEME,KATI YA WATU,YUKO WAPI MUNGU WAO? 18 HAPO NDIPO BWANA ALIPOONA WIVU KWAAJILI YA INCHI YAKE AKAWAHURUMIA WATU WAKE.19 BWANA AKAJIBU,AKAWAMBIA WATU WAKE;TAZAMENI,NITAWALETEA NAFAKA,NA DIVAI,NA MAFUTA,NANYI MTASHIBA KWA VITU HIVYO;WALA SITAWAFANYA WAKE; LA KASKAZINI NITALIONDOLEA MBALI NANYI,NAMI NITALIFUKUZA MPAKA INCHI YA UKAME NA UKIWA;SEHEMU YAKE YA MBELE ITAINGIA KATIKA BAALI YA MAGHARIBI;NA UVUNDO WAKE UTAPANDA JUU,NA HARUFU YAKE MBAYA ITAPANDA JUU,KWA SABABU AMETENDA MAMBO. 21 Ee INCHI USIOGOPE; FURAHI NA KUSHANGILIA, KWA KUWA BWANA AMETENDA MAMBO MAKUBWA.AMEN! ungependa kuwasiliana nami kwa ushauri na maombi karibu Nipigie kwa 0612083598 au niandikie pastorvictorykiluguma@blogspot.com Amen Bwana awabariki sana
Monday, July 22, 2024
MKUTANO WA INJILI IRINGA
AGAPE PENTECOSTE JERUSALEMU CHRISTIAN CENTRE KITAYAWA IRINGA.KWA ASKOFU VICTORY KILUGUMA. TUNAYOFURAHA KUWAKALIBISHA NYOTE KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UTAKAOFANYIKA TAR 8/8/2023/HADI TAR 11/8/2023 BWANA AWABARIKI SANA