Friday, September 13, 2024

MAFUNZO YA UONGOZI NI MSINGI MKUBWA KATIKA KUJENGA MAISHA BORA YA KIKRISTO

 Shalom wa pendwa katika Yesu kristo mwokozi wetu.  Kitabu cha kwanza na cha pili cha Timotheo ni vitabu vinavyo funua ukweli kuhusu uongozi wa kichungaji.   Nyaraka hizi mbili zinatuonesha wachungaji watumishi wa Yesu kristo ambao wamefundishwa na Mungu kukaa katika kweli ya Neno la Mungu.             1tim 3:15 mtume Paulo anamwambia Timotheo nakuandikia upate kujua jinsi iwapasavyo watu  kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Mtume Paulo anasema na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha wengine " 2tim 2:2. Katika safari ya kwanza ya umisheni,Paulo alienda katika mji uitwao listra. Huko alikuwako kijana aliyekuwa akiishi huko aliitwa Timotheo. Paulo mtume akakutana naye kijana Timotheo pamoja na familia yake. Bibi na mama yake Timotheo familia hii walimpokea kristo kuwa mwokozi wao.baadae tena katika safari ya tatu huko listra mtume aliitembelea familia ya Timotheo na kumwalika Timotheo kuungana naye katika safari zake za umisheni. Timotheo akiwa kijana mkubwa alikubali kuwa mmishenari pamoja na Paulo mtume, Paulo akamwita Timotheo nakuwa kijana wake Paulo katika imani maana, alimwongoza kumfahamu Bwana.   Paulo mtume alimpenda kijana Timotheo alikuwa kijana aliye mwamini Mungu imani iliyotokana na bibi yake na mama yake 2tim 1:5- baadae anajifunza kumtumikia Bwana kutoka kwa Baba wa kiroho mtume Paulo. Timotheo alikuwa na mwonekano mzuri kwa watu waliomwani Mungu katika mji wa listra na watu walimshuhudia mema. Mate 16:2 baadae sana mtume paulo akiwa gerezani anamwandikia waraka akikumbuka huruma na upendo wa kweli aliokuwa nao kijana Timotheo. mtume Paulo alifurahi mno alipomkumbuka Timotheo. 2tim 1:4. Baadae Paulo anatoka gerezani anamchukua Timotheo anamfundisha kumtumikia Bwana anasafiri naye katika huduma. Timotheo anamwona mtume Paulo akihubiri injili na kufundisha wakristo wapya. na kuwaongoza katika kweli yote ya Mungu. Timotheo anamwona mtume Paulo ni baba wa kiroho na Mwalimu wake wa imani. Mtume Paulo alifungua makanisa mapya, akiwafundisha wakristo wachanga kiroho akiwaimarisha katika imani na kuwaongoza. Mtume Paulo anamwona Timotheo ni kijana anaye penda kujifunza,anafuata kanuni ya imani, ni mwaminifu,katika mafundisho, mtume Paulo anamweka Timotheo kuwa mchungaji wa kanisa la efeso. Kazi ya Bwana aliyo kabidhiwa Timotheo ilikuwa ikiendelea kukua, Paulo na Timotheo wakaendelea kumtumikia Mungu pamoja kwa upendo kama baba na mwanae. Katika imani ya kristo. Timotheo alibaki katika mji wa efeso akifundisha na kuchunga kundi la Mungu. katika siku zile kulikuwa na hatari maana walitokea watu waliojifanya waalimu wa uongo 1tim 1:6-7 waliamu hawa walifundisha uongo. Kwa sababu hii alihitajika mtu ambaye angeweza kuwazuia, na kufichua hila yao, kwa kuwafundisha watu wa Mungu Neno la Mungu kwa usahihi kabisa.ili watu wote waijue kweli yote ya Mungu. Paulo anamwona mchungaji Timotheo angeweza kufanya hivyo. 1 tim 1:3-4. Mtume Paulo anasisitiza wetu waishike ile imani ya kweli.   Ni jukumu la kila mchungaji kuliongoza kanisa, katika kweli, ya yote ya Mungu. Ni lazima mchungaji aihubiri injili ya kweli kwa uaminifu, na zaidi sana lazima mchungaji aiishi hiyo kweli mbele za Mungu na watu anaowaongoza. Haleluya! watu wa Mungu! Naami ujumbe huu utafanyika baraka kwako! Bwana awabariki nyote. Mtayarishaji ni mimi mtumishi wa Mungu Victory chalres kiluguma kutoka Agape sanctuary christian pentecoste Jerusalem lringa. Ungependa kuwasiliana nami niandikie; pastorvictorykiluguma@blogspot.com au victorykiluguma80@gmail.com au nipigie simu 0612083598. Amen!

Sunday, September 1, 2024

Picha nzuri pastor victory














 Pichani nikiwa Kilimanjaro kwa umisheni mjini na vijijini watu wengi wakamwamini Bwana.